Letra de Leah
Letra powered by LyricFind
Leah - Dully Sykes / Tanzania
Nilimkuta Leah amejilaza
Chini kwenye kituo cha wamataa
Huku ngozi yake maji ya kunde
Imegeuka ya majani isiyopendeza
Unafanya nini nikamuliza ?
Akanijibu anaumwa na pia ana njaa
Msichana wa miaka wa kumi na tisa
Kumbe alikuwa amesha hadhirika
Nikampeleka duka la madawa
Hili kidonge kidogo imweke sawa
Kwani alikuwa na fungus mwili mzima
Ikambidi anihadhithia stori nzima
Akaanza kuniadhithia kwa huruma
Kwamba siku mmoja alikuwa anatoka shuleni
Siku hiyo njaa ilimtawala
Akotokea dereva wa daladala
Akamwambia Leah Lifti panda mbele
Japo mwanafunzi akae kiti cha mbele
Tena bila malipo ni burebure
Akaanza kumtongoza polepole
Sababu Leah njaa ilimtawala
Akaambiwa atanunuliwa Chipsi, Soda
Ilipofika jioni akanunuliwa
Wakapanga wakutane tena
Palepale
Ilipofika
Wakakutane palepale
Akapanda daladala hadi usiku
Wakaenda kufanya yao mavitu
Wakaenda kufanya yao mavitu
(Refr) Leah
Umekwenda
Hayo yote Mola amepanga 3x
Akamrubuni nakumfanya mapenzi
Akawa akitoka schule yeye kwa mchizi
Kwa bahati Leah schule alimaaliza
Baada ya tu kumaliza akatoroshwa
Akaishi na yeye
Kama mke na mume
Nyumbani alikuwa na magokumu yote
Kuosha viombo kupika na khadhalika
Ikawa akikosa kidogo anapigwa
Baada hema na mume akawa na kisirani Alivumilia mpaka mwisho akashika mimba
Alikaa nayo mpaka miezi tisa
Aliyifungulia huko muhindili
Mtoto akafa baada ya miezi miwili
Alikufa kwa ugonjwa wa Nimonia
Baadaye pia aliuguwa
Alikuwa na tatizo la kifua
Tubercolosis oh liliyomsumbuwa
Muda wa wiki mbili alisumbuliwa
Ilipofika Tarehe sita mwezi wa kumi
Nakumbuka siku hiyo ilikuwa jumapili
Ndiyo siku hiyo Leah alifariki
Ilipofika jumanne tarehe nane
Ikabidii watu wote tuungane
Tukamzika tabata makaburi
Hapo ndipo yalikuwa makaburi
Mungu mlaze mahali pema peponi x 2
Leah
Letra powered by LyricFind